Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Tunaboresha taswira ya jengo: Ofisi za Makao Makuu TIRA mbioni kukamilika
05 May, 2025
Tunaboresha taswira ya jengo: Ofisi za Makao Makuu TIRA mbioni kukamilika

Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), lililopo jijini Dodoma eneo la Njedengwa lipo katika hatua za mwisho kukamilika ambapo Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma – TIRA leo Mei 5, 2025 kimetembelea jengo hilo.

Ziara hiyo imelenga kuhakikisha kuwa taswira ya TIRA inaakisi maono yake, majukumu yake na mikakati yake mbalimbali. 

Azma ya TIRA ni kuhakikisha muonekano wa Ofisi hiyo unakuwa nadhifu na wenye kupendeza katika kuhudumia  wadau mbalimbali.

Muonekano wa chapa madhubuti husaidia kutoa ujumbe unaoeleweka kwa haraka, kuimarisha utambulisho wa taasisi, na kuleta mvuto kwa wadau mbalimbali wakiwemo kampuni za bima, watumiaji wa huduma na washirika wa maendeleo.

Jengo hilo sio tu lina ofisi za kutosha kwa watumishi wake bali pia kumbi mbalimbali za mikutano na sehemu za kupumzika kwa wadau mbalimbali wakiwemo wananchi ambao TIRA ina jukumu kubwa la kuhakikisha wanapata huduma stahiki kwa wakati na haraka. 

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA