Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu TIRA ang’ara tuzo za Wafanyakazi Hodari wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala 
23 Jul, 2025
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu TIRA ang’ara tuzo za Wafanyakazi Hodari wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala 

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu TIRA ang’ara tuzo za Wafanyakazi Hodari wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala - 

Leo Julai 23, 2025 Bi. Hawa Mniga, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu TIRA, ametunikiwa cheti maalumu, ishara ya kutambuliwa kwa mchango wake katika kukuza sekta hiyo nchini, huku akipeperusha bendera ya Mamlaka vilivyo.  Tunuku hiyo imefanyika katika Mkutano Mkuu wa Kwanza Jumuishi wa Wataalamu wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala katika Utumishi wa Umma (TAPA – HR) unaondelea katika ukumbi wa AICC jijini Arusha ulioanza Julai 22 na kutarajiwa kumalizika Julai 25, 2025. 

Aidha cheti hicho kilisomeka maneno yafuatayo yakiashiria ufanisi, nidhamu na weledi; “Kwa mchango wako wa kipekee katika eneo la Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu. Ujuzi wako wa hali ya juu, kujitolea kwako na dhamira ya kufanikisha mambo kwa ubora umechangia kwa kiwango kikubwa mafanikio katika Utumishi wa Umma. Tunathamini bidii ya kazi yako na mchango wako chanya uliotukuka”. 

Bi. Mniga, amehudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya Utumishi wa Umma kwa zaidi ya miaka ishirini sasa, akiwa na ujuzi wa kutosha katika sekta hiyo na uzoefu anaoutumia sasa ndani ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania katika eneo hilo la Rasilimali Watu na Utawala linalofanya vizuri. 

Mkurugenzi huyo amepokea salamu mbalimbali za pongezi kutoka kwa Kamishna wa Bima, Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka hiyo.

#Rasilimali Watu na Utawala katika Utumishi wa Umma
#Kazi na Ushindi 
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA