Maonesho ya Nane Nane 2025 sasa kitaifa Dodoma; TIRA tunashiriki

Maonesho ya Wakulima 2025 maarufu kama Nane Nane ambayo yanafanyika kitaifa jijini Dodoma yamezinduliwa rasmi tarehe 1 Agosti 2025 na Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Philip Mpango katika viwanja vya Nzuguni jijini hapo, ambapo TIRA tunashiriki.
Aidha,katika banda la TIRA kuna madawati matatu kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi likiwemo dawati la usajili, malalamiko na dawati maalumu kwa ajili ya kutoa elimu ya bima. Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ina lengo la kuongeza uelewa wa masuala ya bima kwa wananchi kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2030 hivyo maonesho yamekuwa sehemu muhimu ya kutoa elimu ya bima kufikia malengo hayo.
Meneja wa TIRA kanda ya Kati Bw. Frank Shangali ametoa rai kwa wananchi wa Dodoma kushiriki kwa wingi katika banda la Mamlaka lililopo upande wa mabanda ya Serikali, banda namba 1, ili waweze kupatiwa elimu ya bima ikiwemo bima ya kilimo na ufugaji namna inavyoweza kukinga mali hizo. Kampuni za bima zinazotoa bima za kilimo pia zinashiriki.
Wananchi wote mnakaribishwa.
#Karibu maonesho ya nanenane
#TIRA kwa soko salama la bima