Kijiji cha Bima tena Saba Saba – Una changamoto ya kibima? TIRA, kampuni za bima; Tupo kukusikiliza, karibu upate elimu

Unataka kukata bima na haujui uanzie wapi? TIRA tuna habari njema kwako mkazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani, karibu kwenye banda letu, “Kijiji cha Bima” katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Saba Saba ambapo TIRA na wadau wake wakiwemo kampuni za bima wamekusanyika lengo likiwa kutolewa kwa elimu ya bima kwa watanzania lakini pia kutolewa kwa huduma za bima.
Tupo sehemu gani viwanja vya saba saba? Banda letu lipo mkabala na banda la Wizara ya Viwanda na Biashara pia ni banda linalofuata baada ya banda la TTCL ukiwa umetokea upande wa geti la kuingilia viwanjani.
Ewe Mwananchi tunakukaribisha upate elimu ya bima, ufahamu majukumu yetu kama kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima, kuandaa kanuni na miongozo katika soko la bima, kuishauri Serikali juu ya masuala ya bima, lakini pia ujifunze wajibu wetu TIRA kama msimamizi wa Bima ya Afya kwa Wote.
Maonesho haya yameanza rasmi tarehe 28 Juni 2025 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 13 Julai 2025 karibuni nyote.
Karibuni sana Kijiji cha Bima, TIRA kwa Soko salama la bima
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA