Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Kateni bima za afya, gharama nafuu matibabu bila kikwazo
15 Feb, 2025
Kateni bima za afya, gharama nafuu matibabu bila kikwazo

Leo tarehe 12 Februari 2025 Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania imeshiriki katika Kongamano la kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) llilofanyika BAKWATA Makao Makuu Kinondoni, Dar es Salaam.

Kupitia Kongamano hilo Mamlaka imetoa elimu ya bima kwa ujumla na kusisitiza juu ya kila mtanzania kuchukua hatua ya kukinga kila anachokithamini vikiwemo afya na mali kupitia bima.

Akimuwakilisha Kamishna wa Bima Tanzania Bi. Hadija Maulid, Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa TIRA amesisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na bima hususan bima ya afya kwa kuwa sasa sheria ya bima ya afya kwa wote ya mwaka 2023 imeshaanza kutekelezwa.

“Nawasihi ndugu zangu wekeni kinga kwa ajili ya afya zenu kwa kukata bima ya afya kwenye kampuni na mashirika mbalimbali yaliyosajiliwa na TIRA, Bima hizi za afya mtakazokata kwa gharama ndogo zitawasaidi nyie na familia zenu kupata matibabu bila vikwazo vya kiuchumi utakapougua kwa kuwa tayari ulishachangia awali”

Awali Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Ally Ngeruko aliwashukuru TIRA na sekta ya bima kwa jumla kwa kuwapatia Watanzania wenye uhitaji bima za afya 1093 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Kamishna wa Bima Tanzania kutoa bima 10,000  kwa Watanzania wenye uhitaji kupitia Mufti.

Zoezi hilo linaendela kutekelezwa kwa awamu ili kuhakikisha lengo lililowekwa linatimia la kugawa bima Elfu kumi linatimia. 

Katika kongamano hilo Kampuni ya Bima ya Assemble imeshiriki kutoa huduma mbalimbali za bima ikiwemo elimu na upimaji wa afya.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA