Kamishna wa Bima Tanzania afanya ziara mkoani mwanza; uhamasishaji wa bima
03 Mar, 2025

Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware na ujumbe wamekutana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Said Mtanda na Katibu Tawala wa mkoa huo, Bw. Balandya Elikana wakati wa ziara ya kutoa elimu ya bima leo Machi 3, 2025.
Ziara hio imelenga kuhamasisha wakuu wa mikoa, makatibu tawala na watumishi wa umma kuhusu umuhimu wa bima, kuwahamasisha watumishi wa umma kuhusu fursa za kuwekeza zilizopo katika sekta ya bima na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.