Naibu Kamishna Bima Nchini Bi. Khadija Said amewataka wananfunzi nchini kusoma kwa bidii ili wawe tunu ya Taifa huku akiwahusia kuchukua masomo yanayoendana na masuala ya bima.

Bi. Khadija alisema hayo wakati wa ziara ya mafunzo ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Boabab ilipotembelea ofisi ndogo za Mamlaka ya Usimamizi wa Bima jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Mkuu huyo aliwaambia wanafunzi hao kuwa sekta ya bima bado ina fursa nyingi ambazo zinawategemea wasomi mbalimbali ili kuweza kuendesha sekta hiyo.

Bi. Khadija alisema sekta ya bima ina fursa nyingi za ajira ikiwemo kuajiriwa katika makampuni ya kutoa huduma za bima lakini vilevile kuna wigo mpana wa kujiajiri mwenyewe endapo mtu ana taaluma za bima.

Mwalimu aliyeogozana na wananfunzi hao Wanafunzi wa shule hiyo Ester Mwakalinga aliishukuru Mamlaka kwa kutoa mafunzo kwa wananfunzi ambayo yamesadidia kufahamu masuala mbalimbali ya bima lakini pia kujibu maswali mengi ambayo walikuwa wanajiliza kwani wana masomo ambayo yanagusa taaluma ya bima.

Ziara kama hiii ni sehemu ya mkakati wa TIRA wa utoaji elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili waweze kufahamu mambo ya bima, hii huenda sambamba na kuanzisha Klabu za Bima mashuleni (insurance clubs), vipindi vya radio na televisheni.