Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Karibu

Salaam Watumiaji wa Tovuti ya Mamlaka

Karibuni na kwa mara nyingine niwashukuru kutembelea tovuti yetu yenye nia ya kuhabarisha mambo mbalimbali kuhusu sekta ya bima nchini lakini pia kuelezea utendaji wa Mamlaka. Kama mnavyoona katika tovuti hii, Mamlaka imezidi kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi wanaotaka kuwekeza katika biashara ya bima ikiwa ni lengo la Serikali la ushirikishwaji wa Wananchi katika masuala ya kifedha kwa ujumla.

Mamlaka pamoja na wadau wa sekta ya bima inatekeleza Mpango wa Serikali wa Kukuza Sekta ya Fedha 2020/2021 – 2029/2030. Katika mpango huu, sekta ndogo ya bima ina jukumu la kuhakikisha huduma za bima zinawafikia Wananchi kwa wingi kufikia kiasi cha asilimia 80 ya Watanzania ifikapo mwaka 2030.

Katika kuchukua hatua za kutekeleza maagizo hayo, hivi karibuni Mamlaka imetoa miongozo (imepandishwa katika tovuti hii) ambayo ikitumiwa na watoa huduma za bima nchini, Wananchi na wawekezaji mbalimbali itaweza kufanya lengo la Serikali la kukuza sekta ya fedha litafikiwa kwa mwaka huo.

Mamlaka itaendelea kujenga mazigira bora kuhakikisha huduma ya bima inapatikana kwa haraka, weledi, kufikisha huduma vijijini na kwa gharama nafuu. Hata hiyvo, haya yote yataweza kufanikiwa ikiwa wadau mbalimbali watahakikisha soko halina udanganyifu, likiwa la ushindani, weledi na lenye kutengeneza faida kwa wawekezaji.

Asante na Karibuni